SERIKALI kupitia taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) imeandaa mpango wa kujenga redio jamii katika halmashauri ya wilaya ya Madaba.
Hayo amesema Naibu Waziri wa habari,Mawasiliano na teknolojia ya habari Maryprica Mahundi katika ziara yake ya siku moja katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba ya kuangalia mawasiliano.
“Sisi Wizarani kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) tunautaratibu wa kujenga redio jamii, lakini Mbunge wa Jimbo la Madaba alileta ombi na tayari linachakatwa tumuombee Rais tupate hela ,Mkurugenzi tutakuja kuwafungia Radio jamii wananchi wote mtaisikia”.
Mhandisi kutoka taasisi ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) Shirikisho Mpunji amesema shirika hilo linawezesha kufikisha mawasiliano ya simu na redio maeneo ya vijijini.
“Tumefika madaba tumeona kunachangamoto kutokana na mnara uliojengwa unatumia sola kama jua hakuna unazima tumekuwa tunawashauri watoa huduma wawe wanapeleka umeme wa tanescol”.
Aidha amesema wanamabada wasiwe na hofu kuna mradi umeandaliwa na Wizara kwaajili ya kujenga minara 636 nchini na Madaba itajengwa minara mitano.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 16,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa