SERIKALI ya awamu ya sita imedhamilia kuboresha mawasiliano katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kujenga minara mitano ya mtandao wa simu katika kata tano.
Hayo amesema Naibu Waziri wa Habari , Mawasiliano na teknolojia ya habari Maryprisca Mahundi katika ziara yake aliyotembelea kata Wino,Matetereka,Mkongotema na Gumbiro iliyojumuisha vijiji 8.
Mahundi amesema lengo la ziara yake ni kujionea sura ya mawasiliano vijijini yanaimalika Tanzania nzima na siyo mjini pekee.
“Nyie ni mashuhuda ni miradi mingi ya maendeleo mmeletewa, Mhe. Rais anataka kuhakikisha Tanzania nzima hadi pembezoni lazima kasi ya teknolojia ya habari iendane na miundombinu na iimarishwe”.
Kwa upande wake mhandisi kutoka taasisi ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) Shirikisho Mpunji amesema kazi yao ni kushugulika na maeneo ya vjijini ambayo yana changamoto ya mawasilino.
“Nimefika hapa nimeona changamoto tulitarajia mnara uliopo lilondo ungeweza kufika wino kulingana na hali ya kijiographia iliyopo Wino tutawajengea mnara wenu uweze kuwatosheleza “.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 16,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa