SERIKALI imeleta fedha kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 560 kwaajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Lilondo.
Shule hiyo inajengwa kupitia mradi SEQUIP na imefikia hatua ya upigaji wa plasta majengo yote na kutarajia kukamilika mwanzoni mwa Mwezi Disemba 2023.
Mhandisi wa Mkoa wa Ruvuma Girbert Simya na timu yake walipotembelea mradi huo wameshauri kuhakikisha wanachimba mashimo ya vyoo kabla ya mvua kuanza na kuendelea kukamilisha kwa ubora hasa katika vitasa vya milango kwa wakati uliopangwa.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmshauri ya Madaba
Novemba 19,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa