WAKALA wa Maji Vijijini (RUWASA) wameshirikiana na Jumuiya ya watumia Maji JUALULU,pamoja na Kikundi cha kutunza Mazingira cha Tazama Halmashauri ya Madaba wamepanda Miti 500 katika chanzo cha Mto Madaba.
Mhandisi Sheila Kimweli katika zoezi hilo amesema wamepanda miti hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha wanavilisisha vizazi vijavyo.
Kimweli ametoa wito kwa wananchi wote kuhakikisha wanatunza mazingira ili kuhakikisha wanaboresha kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 inayosema Tunza mazingira,okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake afisa Mtendaji wa kijiji cha Madaba Stephano Lungu amesema kwa kutambua umuhimu wa utunzaji wa Mazingira ameungana na kikundi cha Tanzama kupanda miti katika eneo la Mto Madaba.
Lungu ametoa rai kwa wanahanchi kuhakikisha wanashiriki zoezi la upandaji miti na kutunza mazingira kila iitwapo leo ili kuhakikisha mazingira yanaboreshwa.
“Napenda kuwahamasisha wananchi utunzani wa mazingira na kupanda miti nawasihi upandaji wa miti ni muhimu sana kwa afya “.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa