Mkoa wa Ruvuma umefanya jitihada za kuimarisha na kuongeza thamani ya Maziwa katika Halimashauri zake.
Afisa Mifugo Mkoa wa Ruvuma Nelson William amesema wamefanya uchunguzi wa Magonjwa kifua kikuu (TB) na ugonjwa wa kutupa mimba (brucellosis) kwa Ng’ombe wa maziwa 1,546.
Amesema katika Halmashauri za Wilaya ya Namtumbo,Songea na Manispaa ya Songea Mkoa umehamasisha wasindikaji wadogo wadogo wa Maziwa kwa sasa kuna jumla ya wasindikaji 6 wanasindika kwa wastani wa lita 201,600 kwa mwaka.
Hata hivyo Afisa Mifugo amesema mfumo wa utambuzi na ufuatiliaji wa Mifugo Tanzania unasimamiwa kwa Sheria ya Usajili Na 12 ya Mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011.
“Kwa Mkoa wetu wa Ruvuma Halmashauri ziko kwenye hatua tofauti ya maandalizi ya kutekeleza zoezi hili”.
Amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Mkoa wametoa Elimu kwa Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri,Wakuu wa Idara za Mifugo na Uvuvi Maafisa Tehama pamoja na Maafisa Utambuzi wa Halmashauri.
Afisa mifugo amesema zoezi la utambuzi litasaidia kudhibiti wizi wa mifugo pamoja na kuthibitisha umiliki wa mifugo hiyo ikiwemo fursa ya kibiashara ya Kimataifa kwa kukidhi viwango vya ushindani na soko la kimataifa.
William amezitaja changamoto katika Sekta ya Mifugo ikiwemo Ukame maeneo ya ranchi ndogo na ukosefu wa miundombinu ya maji Majosho pamoja na ukosefu wa kudhibiti Magonjwa kliniki za mifugo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 16,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa