Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema udumavu bado changamoto ambapo takwimu zinaonesha Mkoa una udumavu kwa asilimia 35.6.
Kanali Thomas amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa utekelezaji wa mkataba wa lishe uliofanyika katika ukumbi wa Chandamali Manispaa ya Songea.
Amewaagiza waganga wakuu wa Wilaya kuendelea kusimamia utekelezaji wa masuala ya lishe katika afua mbalimbali kuanzia ngazi ya jamii,vituo vya tiba,ngazi ya kata ,vijiji na mitaa.
“Bado hatufanyi vizuri katika eneo la udumavu,Mkoa wetu udumavu ni asilimia 35.6,hivyo lazima mtambue kuwa bado tuna kazi kubwa ya kusimamia afua za lishe katika ngazi ya jamii na vituo vya kutolea huduma za afya’’,alisisitiza.
Amesema kufanyika kwa mkutano huo ni muendelezo wa utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma Septemba 30,2022.
Amesisitiza kuwa Mkoa wa Ruvuma utaendelea kufanya tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe mara mbili kwa mwaka na kwamba Halmashauri zote zitafanya tathimini hiyo kila robo ya mwaka ambapo amewaagiza wakuregenzi watendaji kushirikiana na waganga wakuu kusimamia utekelezaji wa masula ya lishe.
Amewaagiza wakuu wa shule kuhakikisha kila shule inatoa huduma ya chakula kwa uhakika kwa wanafunzi wote badala ya kutoa chakula kwa madarasa ya mitihani yakiwemo darasa la nne,kidato cha pili na cha nne huku madarasa mengine yakipata chakula kwa idadi ndogo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ameagiza kutafutia majawabu ya tatizo la ukosefu wa virutubishi katika vyakula vinavyoliwa shuleni.
Mkuu wa shule sekondari ya Wavulana Songea Mwl.Gerasias Lugome akizungumza kwenye kikao hicho cha tathmini ya lishe,ametoa rai kwa wakuu wa shule na wadau wa elimu kuzingatia utoaji lishe kwa wanafunzi ili kupunguza udumavu ambao ambao unachangia kushusha taaluma shuleni.
Mikoa yenye mitano yenye kiwango kikubwa cha udumavu nchini ni Pamoja na Iringa inayoongoza kwa asilimia 56.6,Njombe asilimia 50.4,Rukwa asilimia 49.8,Geita asilimia 38.6 na Ruvuma asilimia 35.6
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa