• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika

RUVUMA waadhimisha kuzaliwa kwa Dkt Samia kwa kupanda miti

Posted on: January 27th, 2023

Mkuu wa  Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaongoza wananchi  kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupanda miti katika shule za Msingi  na sekondari Mashujaa Manispaa ya Songea.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi hilo,Kanali Laban amesema Mkoa umeamua kuifanya shughuli  ya kupanda miti ya matunda ikiwa ni maalum kuunga mkono siku ya kuzaliwa kwa Rais.

“Nichukue fursa hii kumtakia heri na afya tele Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa,kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma tunampongeza sana,Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda ili aendelea kuliongoza Taifa letu la Tanzania’’,alisema

Amesema mara nyingi Rais Dkt.Samia amekuwa wanahimiza watanzania kupanda miti ya matunda hivyo katika tukio hilo ,Kanali Thomas ameongoza kupanda miti ya matunda aina ya miparachichi na mipera katika shule za msingi Mashujaa na shule ya sekondari Mashujaa.

“Jambo muhimu sio tu kupanda miti,bali kuhifadhi na kuilinda ili miti hiyo iweze kukua,miti hii kwa kuwa ni ya matunda inaweza kutumika kama chakula kwa wanafunzi hivyo kujenga afya za wanafunzi na wal’mu’’,alisema RC Thomas.

Mkuu wa Mkoa amewahimiza wananchi wote mkoani Ruvuma kuendelea kupanda miti nyumbani na kwenye mashamba ambapo amesema mashamba mengi ya kahawa hivi sasa yamebakia vipara baada ya miti kukatwa hivyo amewashauri wakulima kuhakikisha mashamba yao yanapandwa miti.

Amesema uzinduzi wa Kampeni ya wiki ya upandaji miti kimkoa  ilifanyika Januari Mosi mwaka huu ambapo jumla ya miti milioni 1.1 ilipandwa ambapo amesema zoezi la upandaji miti ni endelevu hadi mvua zitakapoishia.

Afisa Maliasili Mkoa wa Ruvuma Africanus amesema kwenye zoezi hilo maalum lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa jumla ya miti 400 imepandwa kati ya hiyo miti ya matunda 200 na miti ya kupanda kwenye mipaka 200.

Mkoa wa Ruvuma  kwa mwaka 2023 unatarajia kupanda miti ya aina mbalimbali zaidi ya milioni nane ambayo inapandwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Taasisi za Serikali, Taasisi binafsi na wananchi.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Januari 27,2023

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA SENSA May 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 10, 2021
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • MSUYA atoa rai kwa Watanzania kuomba ruzuku ya mradi wa utunzaji wa Mazingira

    March 22, 2023
  • TARURA Madaba walivyojenga Daraja la Mawe kwa teknolojia rahisi

    March 21, 2023
  • RAIS Samia atoa Milioni 850 kujenga Nyumba za watumishi 12 Madaba

    March 21, 2023
  • MIWILI ya Rais Samia Madarakani yaboresha miundombinu ya watumishi Madaba

    March 21, 2023
  • Angalia zote

Video

MADABA KUANZA KUCHIMBA MAKAA YA MAWE
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 10

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: info@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa