• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RC:Ruvuma azindua Mradi wa tathimini ya afya ya Udongo

Posted on: May 12th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amezindua mradi wa Tathimini ya Afya ya Udongo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa unazalisha mazao mbalimbali kwa wingi na kuongoza kitaifa kwa uzalishaji wa Chakula kwa miaka mitatu mfululizo.

Ibuge amezitaja changamoto ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma tija ya uzalishaji wa mazao ikiwemo tatizo la afya ya udongo katika baadhi ya maeneo.

Hata hivyo Ibuge amesema  kutokana na tatizo hilo Mkulima anaweza kuzingatia kanuni zingine  zote za kilimo bora bila kupima udongo  na uzalishaji wa mazao kuwa chini ya kiwango.

“Uzinduzi wa mradi wa tathimini ya afya ya udongo Mkoa wetu unaenda kutatua changamoto  kwa kuwaelimisha wakulima kupima udongo na kuboresha udongo itakayowezesha tija ya uzalishaji”.

Ibuge amesema Kampuni ya OCP imepewa jukumu la kupima udongo nchi nzima na Mkoa wa Ruvuma itapima vijiji 100 ili kuimarisha mkakati wa upimaji wa udongo katika Mkoa wa Ruvuma.

Mtafiti wa Udongo kutoka TARI-Uyole Fredrick Mlowe  amsema baada ya kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya Mkoa udongo  hauna afya umefikia kwenye alama nyekundu ambayo inasababisha uzalishaji ambao hauna tija.

Mlowe amesema kupitia uzinduzi huo wa mradi wa tathimini ya upimaji wa afya ya udongo tatizo hilo linaenda kuisha ikiwa  mmea unahitaji virutubisho 13 ambavyo vinasababisha  lishe katika mmea, kutokana na utafiti umeonyesha udongo wa Ruvuma umekosa virutubisho 10.

“Sisi kama Serikali tumetoa mapendekezo kwa kila mampuni yote yanayozalisha mbolea nchini wafanye jitihada za kutengeneza Mbolea zinazoendana na ukosefu wa virutubisho vilivyokosekana katika udongo”.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Kitengo cha Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Mai 12,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa