MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amekagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Mkondo mmoja kupitia mradi wa Boost uliojengwa kwa shilingi Milioni 331,600,000/=
Thomas mara baada ya ukaguzi wa Shule hiyo amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile kusimamia samani zote zinazotakiwa kuwepo madarasani na Ofisi za Walimu bila kuongeza pesa za mapato ya ndani,bembe zote zinazotakiwa zitengenezwe,laps zilizoonyesha nyufa zirekebishwe.
Ameagiza fundi wa kutengeneza madawati alipwe kwa bei elekezi,Milango yote pamoja na madawati yapigwe vanishi na kufanyiwa usafi,malumalu kwenye jengo la utawala zibadilishwe pamoja na chemba zibadirishwe.
“Mheshimiwa Rais anatafuta fedha ni wajibu wetu wote tusimamie miradi marekebisho hayo yawe yamekamilika ifikapo Septemba 30,2023”.
Mkuu wa Mkoa ameagiza wanafunzi ambao wamejaa katika Shule ya Mkongotema kuanzia darasa la pili kuanza kutumia Shule mpya mara baada ya kukamilisha maagizo aliyoyatoa.
“Shule hiyo ni Mpya tutengeneze Mazingira Mazuri maana hii shule ni nzuri na iwe na mazingira mazuri mmekata miti yote ya asili pandeni Miti ya matunda “.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuwa marekebisho aliyoyasema yatafanyiwa kazi kwa wakati.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa