MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Ahmed Abbas Ahamed akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori ametoa maagizo manne ya utekelezaji na kujibu hoja ipasavyo kwa wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Hayo amesema katika kikao cha mapitio ya utekelezaji wa maagizo ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri.
Makori akiyataja maagizo hayo kufuatia kamati hiyo ilitoa maagizo sita yaliyotakiwa kutekelezwa na menejimenti ya utekelezaji wa Halmashauri ya Madaba ikiwa hakuna hoja iliyotekelezwa.
Hivyo Mkuu wa Mkoa ameielekeza Menejimenti ya Halmashauri ya Madaba kushiriki ipasavyo kuandaa majibu ya hoja na utekelezaji wa mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali.
“Sekretalieti ya Mkoa kwa kushirikiana na menejimenti ya Halmashauri mpitie majibu na vielelezo vyote vya hoja kwa hoja kabla ya kuwasilisha CAG kwaajili ya uhakiki”.
Hata hivyo Makori amesema maandalizi ya majibu ya hoja yaanze mapema mara baada ya taarifa ya CAG inapotoa ratiba ya mapitio na majibu na maandalizi ya uhakiki yaratibiwe na sekretalieti ya Mkoa.
“Halmashauri ichukue hatua ya kinidhamu kwa watumishi wanaozalisha hoja na kuona ni jambo la kawaida kwa kuzalisha hoja za ukaguzi”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Aprili 2,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa