MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas leo Januari 8,2024 ametembelea shule mpya ya Msingi Lipupuma iliyojengwa kwa shilingi Milioni 331 na Sekondari ya Lilondo iliyojengwa kwa shilingi Milioni 560 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Lengo la Ziara hiyo kuona wanafunzi wa Kidato cha kwanza waliopangiwa kujiunga mwaka huu 2024 katika Shule ya Sekondari Lilondo na shule ya Msingi Lipupuma ambayo wamegawa wanafunzi kutoka shule ya Mkongotema.
“Tumeona wanafunzi wameanza kukaa madarasani katika shule ya Msingi Lipupuma,maelekezo yalikuwa leo watoto waanze kuingia darasani kabla ya wiki hii kuisha watoto wote wanaotakiwa kujiunga na shule ya Lilondo wawe wemeripoti”.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa Shule ya Lilondo imejengwa madarasa yanayojitosheleza wagawe wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Wino madarasayatimie hadi kidato cha nne.
“Hapa wamepangiwa wanafunzi 118 ambao wataingia katika madarasa haya na madarasa mengine hakikisheni wanafunzi mnawagawa kutoka shule mama ya Wino Sekondari”.
Hata hivyo Thomas amewapongeza wananchi wa Lilondo kwa kujitoa kwa nguvu zao katika kuanzisha shule hiyo na kujenga madarasa ambayo yatatumika kama hosteli kwa wanafunzi pamoja na nyumba za walimu.
“Kilichonifurahisha Rais wa awamu ya sita baada ya kusikia kilio chenu akaamua kuleta mzigo wa Milioni 560 wa kujenga shule nzima na ninyi madarasa yenu mliyojenga kwa nguvu zenu mmeamua kufanya hosteli kwaajili ya watoto watakaosoma katika shule hii hongereni sana”
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa uongozi wa Halmshauri hiyo kuhakikisha wanaweka miundombinu itakayowasaidia wanafunzi kuishi katika hosteli ikiwemo vyoo,bafu na sehemu ya kufulia.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 8,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa