Kufuatia siku ya Januari mosi ni siku ya upandaji wa Miti Kitaifa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thoma ameshiririki zoezi la upandaji wa Miti Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Wilaya ya Songea.
Zoezi hilo limefanyika katika Hospitali ya Wilaya ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed,Watumishi wa Halmashauri pamoja na watumishi wa TFS kutoka shamba la miti Wino.
Meneja wa Tfs Shamba la Wino Grory Kassimir amesema miti iliyopandwa ni kwaajili ya kulinda vyanzo vya maji pamoja na miti ya mbao.
Hata hivyo amesema miche ya miti hiyo inapatikana bure katika shamba hilo ikiwa kila mwananchi anakaribishwa kuchukua ili ahakikishe anapanda katika maeneo tofauti.
Afisa misitu Mustapha Yange amesema imepandwa miti ya aina tatu ikiwemo mipaina,mizambarau,na migwina lengo la upandaji wa miti hiyo inasaidia kulinda mazingira ikiwa kila mwananchi anatakiwa kupanda miti mitano itasaidia kupuguza janga la ukame.
“Kila mwananchi angalau apande miche mitano ambayo kulingana na mabadiliko ya tabia ya nchi itasaidia kupunguza janga la tabia ya nchi ”.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa