MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amemwagiza mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile kuwakamata wazazi ambao hawatapeleka watoto shule.
Hayo amezungumza alipotembele Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kukagua Miradi ya Boost inayojengwa katika Shule sita za Msingi na awali inayogharimu kiasi cha shilingi Milioni 610,300,000/= na miradi ya Swash inayojenga matundu ya vyoo na uwekaji wa miundombinu ya maji taka katika Shule za Msingi 11 kiasi cha shilingi Milioni 436,359,306.
Mkuu wa Mkoa amesema wazazi wahakikishe watoto wanaenda shule akisoma hata kama hatapata ajira akiingia katika Kilimo atalima kwa kitaalam zaidi tofauti na ambae hakwenda Shule.
“Mh. Mkuu wa Wilaya nakuaminia sana watoto ambao hawaendi Shule kamata wazazi Serikali inaleta hela kujenga shule Watoto waende shule Elimu Pekeake ndio itatukomboa”.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesisitiza wananchi kulima kwa kilimo cha kisasa kuhakikisha heka moja kuweka mifuko 3 ya Mbolea itakayopelekea kuvuna mavuno mengi.
Hivyo amesema kwa wakulima kupitia kipindi hiki cha Mavuno kuhakikisha wanaweka chakula na kuimarisha vyama vya ushirika na kuhakikisha wanauza mazao kwa mfumo wa stakabadhigharani.
Amesema katika Halmashauri ya Madaba ardhi yake yanastawi Mazao mengi yakiwemo mazao ya Ufuta,Mbaazi,Soya,Alizeti,Mahindi,Maharage,Tumbaku,pamoja na Tangawizi
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi kuuza Mahindi NFRA kwa bei ya shilingi 700 kwa kilo na kuacha kuuza kwa walanguzi mtaani ambao wanatumia dumla na kuwaibia wananchi.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai 1,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa