MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas ametoa rai kwa viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanapanda miti ya Matunda katika Mazingira ya Shule.
Hayo amezungumza alipotembelea shule Mpya ya Msingi Lipupuma iliyojengwa kwa shilingi Milioni 331 kupitia mradi wa BOOST na Shule ya Sekondari ya Lilondo iliyojengwa kwa shilingi Milioni 560 kupitia mradi wa SEQUIP.
“Shuleni sitaki ipandwe miti ya mbao,nataka tupande miti ya Matunda tunamaeneo kubwa maparachichi yanastawi,machungwa,mapapai,ili watoto wale kwasababu tunatatizo la udumavu”.
Thomas amesema ulaji wa kujaza tumbo siyo mlo kamili kwa afya ya binadamu hivyo tuhakikishe tunabadilisha mawazo kwa kizazi ambacho kipo shuleni.
“Mtu mwingine anaweza kuona mtoto wangu anakua vizuri anacheza kumbe anaudumavu na kuna wengine udumavu umetoka kwa wazazi,tunafuga kuku nyumbani hatuli mayai,na tukianza kupanda miti mashuleni itasaidia watoto wetu”.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema zoezi la upandaji miti litazinduliwa Januari 19 na kampeni hiyo itapelekea kila mwezi upandwe mti wa matunda katika eneo la Shule.
Amesema kipimo cha mtoto mwenye udumavu anakuwa mgumu kuelewa darasani walimu wanapofundisha hilo linapelekea hata watu wazima kutoelewa wanapoelekezwa jambo.
“Najua ningekuja kipindi cha kiangazi ningekuta watu wengi sana tunapoenda mashambani tukumbe kwenda na vyakula vya watoto wetu”.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kuhakikisha kila mzazi anachangia chakula kwa mtoto wake anapokuwa shuleni.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januri 8,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa