MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas akiwa mgeni rasmi katika Sherehe ya wanawake Duniani amekemea mira potofu zinazowakandamiza wanawake.
Maadhimisho hayo Kimkoa yamefanyika Katika Wilaya ya Nyasa na Kauli mbiu katika sherehe hizo ikisema ubunifu wa mabadiliko ya Teknolojia chachu katika kuleta haki na usawa wa kijinsia.
Thomas amesema kauli mbiu hiyo inasisitiza umuhimu wa mawazo ya ujasiri yenye kuleta mabadiliko Teknolojia jumuishi,ubunifu Elimu na uweza wa kupambana na ubaguzi wa kutengwa.
“Swala la haki na usawa siyo fadhila ni matakwa ya wazi kikatiba chini ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya 1 sehemu ya 3 ibara ya 12 na 13”.
Hata hivyo amesema pamoja na kuwa bado kuwa kuna mira potofu ambazo zinaendelea kuwakandamiza wanawake kusababisha kutokuwa haki na usawa katika kaya maskini kwa miaka mingi.
Thomas amezitaja sababu za wanawake kuendelea kubaki maskini ikiwa moja wapo ni katika kuumizwa katika umiliki wa rasilimali,kukosa dhana ya kuwawezesha upatikanaji wa huduma za kifedha,haki ya kupata Elimu,haki ya kuchaguliwa kuwa viongozi ndani ya jamii na hata haki ya kuchagua mume.
“Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imesimamia katika kulinda haki ya kujenga usawakwa jamii zote na kuhakikisha wanawake wanapata haki kwa kwa kujiamini na kushika nafasi mbalimbali”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasilino Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Februari 8,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa