MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kupata hati safi Miaka sita mfululizo.
Hayo amesema katika kikao maalumu cha baraza la Madiwani cha kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi katika Halmashauri hiyo.
“Hati safi ni ushirikiano na mshikamano huleta matokeo ya utendaji kazi mzuri wa Mkurugenzi na Wataalam pamoja na Madiwani”.
Hata hivyo ameishauri Halmashauri hiyo kuongeza bidii katika utendaji kazi na kuhakikisha wanaendelea kupata hati safi katika ukaguzi ujao.
Kanali ameagiza uongozi wa Halmashauri kuhakikisha hoja na mapendekezo yote yaliyotolewa na CAG yanafungwa kabla ya Septemba 30 mwaka huu pamoja na kuzuia hoja zinazojirudia mara kwa mara.
“Waheshimiwa Madiwani Pamoja na Mkurugenzi wachukulieni hatua za kinidhamu watumishi wote wanaozalisha hoja,kama kuna mtu yoyote amezalisha hoja na amehamishwa arudishwe kwaajili ya kujibu hoja hizo”.kauli yake Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa ameendelea kuagiza kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za manunuzi pamoja na kulipa madeni ya wazabuni.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Juni 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa