• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RC Ibuge aipongeza Halmashauri ya Madaba kwa kupata Hati safi miaka minne mfululizo

Posted on: June 19th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge  ameipongeza Halmashauri ya Madaba kwa kupata hati safi miaka minne mfululizo.

Hayo amesema katika kikao maalumu cha Balaza la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Baada ya pongezi nilizozitoa niseme tena ukweli kuwa matokeo ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2020 Halmashauri ya Madaba mmefanya vizuri sana na mmepata hati safi”.

Hata hivyo ibuge amesema hayo nimatokeo ya utendaji wa kazi nzuri yenye mshikamano na ushirikiano kati ya wataalamu wa Halmashauri na Mkurugenzi pamoja na waheshimiwa Madiwani.

“Napenda niwakumbushe kuwa kupata Hati safi miaka mine mfululizo siyo jambo dogo ni jambo kubwa sana tena la mfano Hongereni sana! hivyo naomba niwape shime kwa kupata hati hizo kuwafanye muongeze bidii katika utendaji wa kila siku kwa lengo la kuhakikisha Hati safi zinaendelea kupatikana Madaba”.

Ibuge ametoa maagizo kwa Halmashauri hiyo kuhakikisha kufunga hoja zote ambazo hazijafungwa kabla ya tarehe 20 septemba 2021 na kupatiwa taarifa kamili ya hoja hizo zilizo jitokeza pamoja na kuzuia hoja zinazojirudia.

Pia wakuu wa Idara washiriki ipasavyo kuandaa majibu ya hoja na utekelezaji wa mapendekezo ya mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu ya Serikali,na Halmashauri ichukue  hatua ya kinidhamu kwa watumishi wanaozalisha hoja pamoja na kusimamia mfuko wa Bima ya afya iCHF iliyoboreshwa na kuhakikisha kila mwananchi anajiunga.

Amesema  ripoti ya Mkaguzi (CAG) kwa mwaka wa fedha 2019/2020 tunaelekea mwishoni mwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambao unaishia tarehe 30 Juni mwisho wa ukaguzi ni mwanzo wa ukaguzi unaokuja amewasihi kujipanga kwa maandalizi ya ukaguzi bila kupoteza sifa ya kuwa na Hati safi.

Mkuu wa Mkoa ameishukuru ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hususani Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na timu yake kwa ushirikiano wanaotoa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma.

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Olaph Pilli akitoa neon la shukrani kwa niaba ya waheshimiwa Madiwani ameahidi kuendelea kufanya vizuri pamoja na kusimamia miradi ya Halmashauri hiyo.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa Habari  Halmashauri ya Madaba

Juni 18,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa