• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RC MNDEME Awaagiza watendaji Serikalini kutatua kero za wananchi kuanzia ngazi ya chini

Posted on: April 15th, 2021

Mkuu wa mkoa Ruvuma Chistina Mndeme  amewaagiza wakuu wa Taasisi serikalini kusikiliza na kutatua kero za wananchi kuanzia ngazi ya chini.

Mndeme ametoa kauli hiyo katika kikao cha kazi cha watendaji na wakuu wote wa Taasisi za  serikali mkoani Ruvuma kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa Songea.

“Mimi kama Mkuu wa Mkoa nimekuwa nikipokea kero mbalimbali ambazo wakati mwingine kero hizo zingetatuliwa katika ngazi ya wilaya au kijiji,nimeona ni vema niwaite wakuu wa Taasisi zote, kwa sababu tunapaswa kutatua kero za wananchi kwenye maeneo yetu’’,alisisitiza.

Amewaagiza watendaji hao kusikiliza kero za wananchi kwa wakati na kuwaagiza kutosubiri kero kuwafikia ofisini badala yake waweke ratiba ya kwenda kwa wananchi kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.

Mndeme ameagiza kila Halmashauri na Taasisi kuunda mkakati wake wa kushughulikia kero za wananchi ili kupunguza kero hizo kuanzia ngazi ya chini.

“Sasa hivi tuna tatizo la mara kwa mara la kukatika kwa umeme,wewe Meneja wa TANESCO kazi yako ni nini,watu wamelipia umeme,hawajaunganishiwa umeme,wewe kama Meneja wa TANESCO  kwanini huendei kwa wananchi na kutoa sababu za kero hizo,tutoe taarifa kwanini maji yamekatika,sio mimi Mkuu wa Mkoa nikatoe taarifa kwa wananchi,tuwasiliane na wananchi’’, alisema Mndeme.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amezitaja sababu mbili kubwa zinaosababisha kero kwa wananchi ni kutokufanyika vikao vya kisheria na wananchi  na kutokuwepo kwa mahusiano mazuri miongoni mwa watendaji wa serikali hivyo ameagiza kufanyika kwa vikao vya kisheria  na kuimarisha mahusiano ndani ya Taasisi za serikali ambayo yatasaidia kupunguza kero kwa wananchi.

“Tukitekeleza majukumu yetu vizuri kwa wananchi,tutaifanya kazi ya Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kuwa nyepesi,sisi ndiyo tupo chini,tutoke maofisini,tusisubiri ziara ya Mkuu wa Mkoa,ninyi wakuu wa Taasisi mnaruhusiwa kwenda kuzungumza na wananchi na kutatua kero zao’’,alisisitiza.

Mndeme ameagiza kila Taasisi kuandaa rejesta ya malalamiko ya ambayo itaratibu malalmiko pia kuunda timu ndogo itakayosaidia kuratibu malalamiko na kuyafikisha kwa mkuu wa Taasisi na kwamba kero za kisera zipelekwe ngazi ya juu ili ziweze kupata utatuzi wa kisera.

Ili kuhakikisha utatuzi wa kero unakuwa endelevu,Mkuu wa Mkoa ameziagiza Taasisi za serikali kila mwisho wa mwezi kufanya tathimini namna kero zilivyoshughulikiwa na kutoa taarifa za kero zinazohitaji ufafanuzi wa kisera kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Ruvuma  Oddo Mwisho amesema ilani ya CCM ya 2020/ 2025 inalitaja moja ya jukumu lake ni kusikiliza malalamiko ya wananchi hivyo jambo linalofanywa na uongozi wa mkoa  wa Ruvuma ni utekeleza wa ilani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amesema katika kushughulikia malalamiko ya wananchi na kwamba hakuna mfumo wa pamoja,hali inayosababisha wananchi kutojua wakimbilie wapi katika kupata suluhu ya matatizo yao.

Ili kuhakikisha kero za wananchi zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu,Mkoa wa Ruvuma umeazimia kuunda timu ya Mkoa ya kutatua kero zinazowakabili wananchi ambayo itakutana kila baada ya miezi mitatu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Aprili 15,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa