• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RC Ibuge azindua uwekaji anwani za Makazi na Postikodi

Posted on: February 15th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amezindua Operesheni ya uwekaji wa anwani za makazi na postikodi .

Uzinduzi huo umefanyika katika Manispaa ya Songea mara baada ya kikao na watendaji wote wa Mkoa huo, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi utekelezaji wa zoezi hilo muhimu.

Ibuge amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maono yake na uamuzi wa kuanzisha operesheni muhimu kwa maendeleo ya Nchi kwa gharama nafuu.

“Kama mnavyokumbuka mwaka 2020 nchi yetu iliingia rasmi kwenye uchumi wa kati Kidunia turejee pongezi za dhati kwa Serikari ya awamu ya tano  iliyoongozwa na Hayati Dr.John Magufuri”.

Hata hivyo Ibuge amesema kuna umuhimu wa kuondoka kwenye Ujima wa enzi za zama za mawe za kupigwa ngoma na kujulishwa ujumbe au taarifa na badala yake Taifa liingie kwenye Zama za  Dunia ya kidijitali na Biashara Mtandao zinazojumuisha matumizi Makubwa ya Teknolojia ya Habari.

Amesema ili uchumi ukue kwa haraka na kuendelea kuwa Jumuishi kama ambavyo sasa Tafiti za Kimataifa zinaonesha kuwa Tanzania ni baina ya Nchi za Afrika zilivyokuwa kinara kwa Uchumi jumuishi ni lazima makazi na biashara ziweze kufikika kirahisi.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi  mkoa wa Ruvuma Ildefonce Ndemela amesema katika sekta ya Ardhi ni muhimu katika utekelezaji wa zoezi la mfumo wa Anwani za makazi na postikodi nchini.

Ndemela amesema mfumo huo ili uweze kuleta tija na ufanisi katika utoaji wa huduma lazima kuwepo na ramani zitakazotumika kuonesha maeneo mbalimbali ya miji na vijiji zizingatiwekwenye mfumo huo.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Feburuari 15,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa