• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RC Ibuge awaapisha Wakuu wa Wilaya Wapya

Posted on: June 22nd, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewaapisha Wakuu wa Wilaya wapya,  nakutoa maelekezo katika utendaji kazi wao.

Hafla  ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya imefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali.

RC Ibuge amewaagiza Wakuu wa Wilaya wahakikishe wanasimamia wananchi kushiriki katika masuala ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao,  kwa sababu hakuna maendeleo bila kuwa Ulinzi na Usalama.

“kasimamieni maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hakikisheni  Miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yenu, inakuwa yenye tija na kukamilika kwa wakati”. alisisitiza RC Ibuge.

 Maagizo mengine aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa kwa Wakuu wa Wilaya ni kuhakikisha Thamani ya fedha katika Miradi ionekana, kuhakikisha uwepo wa   matumizi sahihi ya miradi iliwekezwa na Serikali na kuondoa na vikwazo katika ufanyaji biashara na kuhakikisha hudma inapatikana kwa wakati na haraka.

RC Ibuge pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya  kusimamia uwezeshaji wa Makundi maalum, ambayo ni wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kwa kuhakikisha asilimia 10 ya fedha ya mapato ya ndani, inatengwa kwa ajili ya kundi hilo.

Mkuu wa Mkoa amewataka Wakuu wa Wilaya wakahamasishe wananchi kujiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa, na kuhakikisha Fedha inayotakiwa kununuliwa madawa inawekwa benki.

Amesisitiza kuhakikisha Mazao ya kimkakati  Soya, Ufuta, Mbaazi, Choroko na Korosho Kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, ili wakulima watimize ndoto zao, Pamoja  na kusimamia utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Taasisi za Umma zilizopo katika Halmashauri.

Ibuge amewaagiza Wakuu wa Wilaya  kutatua kero za wananchi, na kusimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi sahihi ya fedha za umma, kusimamia masuala ya Elimu, na matumizi bora ya pembejeo za kilimo na Elimu ya Biashara na ujasiliamali kwa ajili ya kuboresha kipato kwa wananchi.

Kwa upande wake  Mkuu Mpya wa Wilaya  ya Nyasa Kanali  Laban Thomas akizungumza baada ya kuapishwa, amehaidi kuwa Mtumishi, na kutokuwa mtawala  na kujifunza kutoka kwa wananchi pamoja na kuchukua changamoto zao na kuzifanya kuwa fursa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Julius Ningu ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili wanachi wa Namtumbo na anatarajia kujifunza mengi kutoka kwa wananchi wenyewe.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa Habari, Halmashauri Madaba

Juni 22,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa