• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RC Ibuge asisitiza Ushirika kumlinda Mkulima

Posted on: May 31st, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewataka wadau wa kilimo cha kahawa kuendelea kushikamana ili kuongeza uzalishaji, thamani ya soko na kukuza kipato kwa wananchi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa kahawa wa Mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa Manispaa ya Songea leo.

Amesema Mkoa wa Ruvuma umezalisha wastani wa tani 23,000 kwa msimu wa 2021/2022 ambayo imetoa kahawa safi tani 19,152 iliyouzwa hivyo Mkoa wa Ruvuma kwa kuzingatia malengo ya kitaifa umelenga kuzalisha kahawa kavu tani 75,000 itakayotoa kahawa safi tani 60,000 ifikapo mwaka 2025.

‘’Ndugu wadau wa kahawa ili kuhakikisha bei ya kahawa inaongezeka kila mmoja anawajibu wa kufanikisha uimarishaji wa ubora wa zao kwa kadri ya kila mmoja atakavyopaswa kutimiza wajibu wake’’ amesisitiza RC Ibuge.

Hata hivyo RC Ibuge amesema licha ya jitihada za dhati zinazofanywa na wadau wote za kuongeza uzalishaji, bado unywaji wa kahawa upo chini kwa wastani wa asilimia 7 hadi 10 hivyo amewasihi wadau kujijengea mazoea ya kunywa kahawa kwa manufaa ya kiafya.

Kwa upande wake mjumbe wa Bodi ya kahawa ambae amemwakilisha Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa ndugu Gotam Haule amewapongeza wadau wote kwa juhudi kubwa za pamoja wanazozifanya ili kuhakikisha zao hilo linazalishwa kwa wingi.

Mkoa wa Ruvuma umeshika nafasi ya pili kitaifa kwa uzalishaji wa zao zao la kahawa.

Imeandaliwa na Bahati Nyoni na Jackson Mbano

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Mei 30 2022.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa