MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amegawa Vifaa kwa Wakuu wa Wilaya wa 5 kwaajili ya kuhamasisha kujikinga na Corona.
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya wapya amewataka kuwahamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona (UVICO 19).
“Leo nawakabidhi Wakuu wa Wilaya vipaza sauti kwaajili ya utoaji wa elimu kwa jamii ili kujikinga na Ugonjwa huu”.
Akizungumza baada ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,vifaa vya kutolea elimu dhidi ya corona,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dr.Jairy Kanga amesema Dunia hivi sasa ipo katika mapambano makali dhidi ya UVICO 19 hivyo elimu endelevu inatakiwa kutolewa kwa wananchi.
Khanga amesema kuwa tatizo hili bado lipo Afrika, na hata Tanzania hivyo amewaomba waandishi wahabari kutoa taarifa sahihi kuwafikishia wananchi jinsi ya kujikinga na kuchukua tahadhali ya Ugonjwa huo.
“Ugonjwa huo unaambukizwa na vijidudu aina ya Corona ,kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa mate au makohozi ni ugonjwa ambao upo kwenye kundi ya magonjwa ya kuambukiza,mwananchi anapokuwa kwenye misongamano ahakikishe anavaa barakoa”.
Ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo corona kwa kuvaa barokoa wanapokuwa kwenye mikusanyiko na ametoa rai kujiepusha na misongomano isiyokuwa ya lazima.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Juni 23,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa