KAMATI ya Fedha Halmashauri ya Madaba wametembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Igawisenga iliyoghalimu kiasi cha shilingi Milioni 50 kutoka Serikali kuu.
Kaimu Mkuu wa Shule ya Msingi Igawisenga George Karata akisoma taarifa kwa Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Teofanes Mlelwa amesema ujenzi ulianza Januari 2,2023 kwa kutekelezwa kwa force account.
Karata amesema hadi kufikia sasa ujenzi umefikia hatua ya kupaua,kuezeka,blandaring,kufunga dari na skimming ya dari.
Amesema zaidi ya shilingi milioni 43 kimetumika kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya viwandani na visivyo vya viwandani pamoja na malipo ya mafundi na ujenzi huo unatarajia kukamilika Mei 30,2023.
Hata hivyo ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Mwalimu,na Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama pamoja na Diwani wa Kata ya Wino ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa kwa jitihada wananzofanya kuhakikisha wanapata miradi ya Maendeleo.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei,17,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa