RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameleta fedha kiasi cha shilingi milioni 701 katika kijiji cha Wino Kata ya Wino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo amezungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed alipokuwa anasikiliza kero za wananchi wa Kata ya Wino.
“Milioni 701 siyo fedha ndogo katika Kijiji na fedha za Elimu bure pamoja na TASAF ambazo wanaendelea kutoa”.
Hata hivyo amewapongeza wananchi hao kwa ushirikiano wa ujenzi wa miundombinu na kazi nzuri ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Lilondo iliyojengwa kwa shilingi Milioni 560 kupitia mradi wa SEQUIP na kuanza kutoa huduma mwezi Januari 2024.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 26,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa