HALMASHAURI ya Madaba Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma wamepata hati safi kwa miaka mitano Mfululizo tangia kuanzisha kwa Halmashauri hiyo.
Hayo yamebainishwa kufuatia kikao cha Balaza la Madiwani cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika balaza hilo ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kukusanya mapato ya ndani asilimia 89.
“Kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya Mthibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inaonesha Halmashauri imepata hati safi”.
Ibuge amesema miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo imefanya vizuri miaka mitano mfululizo tangu mwaka 2016 hadi 2021.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teophanes Mlewa katika Balaza hilo amepokea pongezi hizo na kuahidi kufanyia kazi hoja zote na kusimamia miradi,mapato ya Halmashauri na kila kitu kiweze kwenda katika kanuni na taratibu.
Mlelwa amesema wamepokea maagizo aliyotoa Mkuu wa Mkoa ikiwemo ni wajibu wao na kutekeleza kwa wakati ili Halmashauri iendelee kufanya vizuri ikiwemo kutatua hoja zinazojirudia.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Juni 30,2020.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa