KUFUATIA kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto Maafisa maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Madaba wametoa elimu katika Shule ya Madaba Day Sekondari na Shule ya Msingi Madaba.
Afisa Ustawi wa Jamii Livin Tarimo akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa Shule ya Sokondari Madaba Day amesema madhara yakufanyiwa ukatili ukiwa mdogo yanaweza kupelekea kuleta matatizo ukubwani.
“Ninyi ni wasomi mnategemewa kutengeneza kizazi cha watu bora leo ni mwanafunzi kesho ni kiongozi ukifanyiwa ukatili wa kijinsia unaweza kuwa mtu wa visasi na hasira”.
Tarimo amewaasa wanafunzi hao kutoa taarifa kwa uongozi husika kama watafanyiwa ukatili na wazazi,au walimu pamoja na watu wengine au kusikia mwenzao kafanyiwa ukatili wa kijinsia na watu wakaribu awebalozi kwa kutoa taarifa.
“Tuanze kutumia Elimu kuanzia sasahivi bila kusubiri kufika chuo kikuu ukifanyiwa ukatili leo ukawa daktari unaweza kuua wagonjwa kwa kudhania kuwa wanaume wote au wanawake wote ni wakatili”.
Juma Komba ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Madaba amewaeleza wanafunzi hao sehemu ya kutoa taarifa endapo watafanyiwa ukatili wakijinsia ikiwemo kwa walimu wa malezi,Dawati la jinsi au Ofisi ya Ustawi wa Jamii pamoja na ofisi za Serikali za Mitaa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Madaba
Novemba 29,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa