AFISA kutoka ofisi ya Viongozi wa Maadali Kanda ya Kusini Samweli Omary ametoa rai kwa Madiwani wakuu wa Idara na watumishi wengine kuzingatia umuhimu wa Maadili katika kazi.
Hayo amezungumza katika kikao kazi cha Baraza la Madaiwa kilichofanyika Januari 31 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ameelezea umuhimu wa maadili kwa Viongozi na watumishi wa Umma.
Omary akielezea umuhimu huo amesema Kiongozi au mtumishi akiwa mwadilifu anaweza kuchambua na kutambua madhara yanayoweza kutokea iwapo kiongozi atafanya maamuzi kwa kuzingatia misingi ya Sheria na maadili.
“Waheshimiwa Madiwani najua mnaitumikia Halmshauri ya madaba ni yenu wataalam waliopo hapa wametoka sehemu mbalimbali wamekuja kusaidiana na ninyi ili kuhakikisha ustawi wa wananchi katika Halmashauri, hamna budi kushirikiana na kufanya kazi kwa mshikamano ndio uadilifu”.
Hata hivyo Afisa wa Maadali amesema Kiongozi au mtumishi mwadilifu lazima ajue mipaka ya majukumu yake na kuwa mtunzaji wa siri juu ya kile ambacho wamejadili na kukubaliana.
“Viongozi na watumishi wale tunao watumikia tuwatumikie kwa uadilifu wa hali ya juu”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 31,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa