SERIKALI imeleta shilingi milioni 200 kwaajili ya ujenzi wa nyumba nne za walimu katika shule ya Sekondari Matetereka Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kupitia mradi wa TEA.
Hayo amesema Afisa Mipango George Magembe katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Madaba kuwa nyumba hizo zitakamilika Septemba 2024 na kuanza kutumika.
Magembe amemponge Mbunge wa Jimbo hilo kwa juhudi kubwa ya kuhakikisha fedha za ujenzi wa miundombinu ya elimu inapatikana na kujengwa kwa ufanisi.
“Sisi kama Halmashauri tunashukuru kwa ushirikiano wako unaotupa,maana tulikushirikisha jamba hili tukaona jitihada zako ukaonana na mkurugenzi wa TEA hatimae tukapata fedha za kutekeleza mradi huu”.
Aidha amesema katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba mradi wa TEA unatekelezwa katika shule ya Matetereka na ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Ifinga kata ya Matumbi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 15,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa