MFUGAJI wa Sugura wa Kisasa kutoa Kata ya Mkongotema Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Meshack Vila ameelezea faidi ya Nyama ya Sungura kwa afya ya binadamu.
Mfugaji huyo anapatikana katika banda la Madaba linapatikana katika viwanja vya Maonnyesho ya Nane nane vya John Mwakangale Mkoani Mbeya amesema Nyama ya Sungura ipo katika kundi la Nyama nyeupo ambayo kiafya ni nyama bora baada ya Samaki,Simbilisi inafuata nyama ya Sungura.
Vila amesema nyama hiyo mara baada ya kula inayeyuka mapema tumboni na inafaa kutumiwa na makundi yote ya binadamu,inaviwango vizuri vya protini na baadhi ya Madini ambayo yanasaidia katika Mwili wa binadamu katika suala zima la ukuaji.
“Kama unavyojua Mikoa yetu ya Kusini inaudumavu tunashauri watu wafuge Sungura ili watoto wapate protini waepukane na hayo matatizo”.
Hata hivyo amesema ufugaji wa Sungura siyo wa kitoto bali ni ufugaji wa maendeleo na uchumi kimsingi kuamua kufuga kwa tija na kwa kisasa.
Amesema ukianza kufuga Sungura 3 majike 2 na dume moja kwa mwaka unaweza kuwa na Sungura 90 hadi 100 kwa mda wa mwaka mmoja.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmshauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 4,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa