MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ameongea na watumishi Halmashauri ya Madaba kwa mara ya kwanza ikiwa ni siku ya tatu kuanza kazi mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas.
Akizungumza na watumishi hao katika ukumbi wa Halmashauri ya Madaba amesema watumishi ni mali ya Serikali wahakikishe wanawatumikia wananchi ipasavyo ili wananchi waweze kufikia malengo yao.
“Serikali inajua mnastahiki zenu haiwezi kuwaacha kwa kuwapandisha madaraja na kuwaongezea mishahara hata mkistaafu mpewe na peshion, Serikali inajua mnawatumikia wananchi lazima muwe katika mazingira mazuri”.
Hata hivyo Ndile amesema ameletwa Wilaya ya Songea kwaajili ya kusimamamia maelekezo ya Serikali kama inavyotaka ikiwa kila jambo litafanyika kama itakavyoelekezwa.
“Serikali imeelekeza kuhusu Elimu Watoto wa awali wanaandikishwe,darasa la kwanza pamoja na anayemaliza darasa la saba aende kidato cha kwanza kazi yangu mimi ni kusimamia”.
Amesema hayo yote yatafanyika vizuri kama kutakuwa na ushirikiano na wazazi,walimu na viongozi wengine ili kila idara iweze kufanya vizuri ikiwa kwa upande wa Madaba Elimu imefanya vizuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akisoma taarifa kwa Mkuu wa Wilaya amempongeza kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea na atahakikisha anapewa ushirikianao na watumishi wa Halmashauri hiyo ili kuhakikisha miradi inayoletwa na Serikali inakamilika kwa wakati.
Mohamed amesema Halmashauri imekuwa inategemea mapato kupitia kilimo pekee kwa sasa imepata wawekezaji wa uchimbaji wa makaa ya mawe katika Kata ya Mtyangimbole ambao wanatarajia kuanza Machi 2023
Amesema Halmashauri hiyo inasimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo ipo iliyokamilika na mingine inaendelea kutekelezwa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Februari 3,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa