MKUU wa Wilaya ya Songea Mh. Pololeth Mgema amesisitiza watalaamu na viongozi wote kuhakikisha miti inapandwa na kutunzwa.
Hayo ameyasema katika Kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili ya mwaka 2022/2023 Halmashauri ya Madaba kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
“Tushirikiane pamoja katika upandaji miti tulianzia Hospitali ya Halmashauri,tukazindua katika Shule mpya ya Lilondo”.
Hata hivyo amesema miti ipandwe katika vyanzo vya maji , na maeneo mbalimbali ikiwa kama sehemu ya kutolea huduma ya afya ipandwe miti ya matunda.
“Nilazima tuisimamie miti hiyo iote kila mwezi tutakagua ile ambayo haikufanikiwa kuota tutairudishia hadi ifikapo aprili maana ni kipindi cha mvua”.
Mwenyekiti wa Halmashauri Teofanes Mlelwa amesisitiza zoezi la upandaji wa miti kwa kuwaagiza watendaji wa vijiji kuleta idai ya miti iliyopandwa katika kila kijiji ili kuhakikisha Madaba inakuwa kinara katika zoezi hilo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Madaba.
Januari 20,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa