• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

NAUYE afurahishwa na zoezi la Anwani na Postikodi Ruvuma

Posted on: April 13th, 2022

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia   Nape Nauye ameupongeza Mkoa wa Ruvuma kwa kasi ya zoezi la uandikishwaji wa anwani za makazi na Postikodi linaloendelea kitaifa.

Akizungumza mara baada ya kusomewa taarifa ya Mkoa na Mtehama wa Mkoa huo Yahya Madenge katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  amesema iko katika asilimia 97.

Nauye amefanya ziara Mkoani humo ya siku moja  na kujionea utekelezwaji wa kasi na kueleza umuhimu wa anwani za makazi kuwa zoezi hilo  litaleta manufaa katika Taifa kwa kuitambulisha Ramani ya Tanzania Kimataifa.

 “Serikali imeona umuhimu wa kufanya zoezi hilo  kwaajili ya kuitangaza inchi ya Tanzania pamoja na  kurahisisha mawasiliano kwa mataifa mbali mbali”.

Hata hivyo Nauye  ametoa wito kwa uongozi wa Mkoa na wananchi kuwa zoezi hilo litumike kuifadhi historia ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla ikiwemo vizazi vijavyo ziweze kujua historia  kupitia majina ya mitaa na Barabara.

Mkuu Mkoa  wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema namna Mkoa wa Ruvuma unavyotekeleza zoezi la anwani za makazi na kufikia asilimia 97 na kushika nafasi ya 10 Kitaifa.

Ibuge amesema katika kuendesha zoezi hilo la anuani za Makazi Katika Halmashauri linatarajia kuisha April 15 na kuwasilisha taarifa kwenyekanzidata na kuweka vibao pamoja na namba kwenye makazi  na Kitaifa April 30.

Ibuge amewapongeza wananchi wa Mkoa huo kwa namna ambavyo wameona ushirikiano kwa kupendekeza majina ya Mitaa yakiwemo ya Viongozi na kujitoa kugharamia pale panapohitaji gharama na kuongeza nguvu kwa kuhakikisha zoezi linakwenda vizuri.

Hizi nguzo tunazoziweka ni zoezi litakalokuwa endelevu, ndugu wananchi wa Mkoa wa Ruvuma zikalindwe tutoke kwenye ujima na ushamba wa nguzo kwa “sababu ni chuma na kuona  chuma chakavu hiyo nayo ni  kipimo kingine ambacho tutakuwa tumejishusha” 

Imeandaliwa na Aneth Ndonde pamoja  Jackson Mbano

Kutoka Kitengo Cha Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

April 13,2022. 

 

 

 

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa