Katibu wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Juma Nambaila amewapongeza viongozi wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Wino Halmashauri ya Madaba kwa kutenga siku ya kuelezea mafanikio yaliyotekelezwa na Chama cha Mapinduzi.
Pongezi hizo amezitoa katika sherehe za mafaniko ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali ya Kata ya Wino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba iliyoghalimu zaidi ya shilingi bilioni 2.
“Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Kata ya Wino wewe na wenzako mmefanya jambo jema sana kutenga siku ya kuelezea mafanikio, sisi tulipewa ridhaa na wananchi hawa mwaka 2020 walipanga foleni kwa kupiga kura kuchagua chama cha mapinduzi”.
Nambaila amesema jambo ambalo wamelifanya la kusoma mafanikio ya Kata ya Wino kuanzia mwaka 2022/2023 na 2023/2024 ni mfano wa kuigwa.
“Ndugu mgeni rasmi kwetu sisi chama, ipo haja ya kusimamia na kuona jambo hili linakuwa ni jambo la kuigwa wananchi wafahamu mafanikio yanayofanywa na chama “.
Kutoka Kitengo cha Mawasilino Halmashauri ya Madaba
Mei 6,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa