NAIBU WAZIRI wa Ardhi Angeline Mabula amewaagiza watumishi wa Ardhi Mkoa wa Ruvuma kuandaa Hati miliki tano kwa wiki kwa lengo la kumwezesha mwananchi wa kawaidi kuongezeze thamani ya Arddi yake.
Hayo amesema katika kikao cha wataalamu wa ardhi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa ya Songea amewaambia wawasaidie wananchi kuwapatia haki kwa kasi ili iwasaidie katika matumizi yao ikiwemo kukopa bank.
“Jambo lingine linalosuasua ni ukusanyaji wa maduhuri ya serikali ambapo kwa Mkoa mzima wa Ruvuma imefikia asilimia 16 tu jambo ambalo lipo chini sana ukilinganisha na hali halisi, leo tupo mwezi wa nane tangia mwaka wa fedha umeanza”.
Kamishina msaidizi wa Mkoa wa Ruvuma Ildefonce Ndemela amesema Mkoa wa Ruvuma katika mwaka wa fedha 2020/2021 umepangiwa lengo la kupima viwanja 16,550 na mashamba 104 mpaka kufikia februari 22,2021 viwanja 4,873 na mashamba 5 yamepimwa katika maeneo ya vijijini kwaajili yamatumizi mbalimbali.
Ndemela amesema Ofisi ya ardhi Mkoa wa Ruvuma tangu kuanzishwa kwake imesimamia na kutekeleza kazi za upangaji, upimaji, umilikishaji, uthamini usajili wa Hati na nyaraka mbalimbali ikiwemo utatuzi wa migogoro ya ardhi na ukusanyaji wamaduhuli ya serikali.
Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2020/2021 Mkoa umepangiwa kukusanya kodi ya shillingi bilioni 4.6 katika Halmashauri 8 za Mkoa wa Ruvuma mpaka sasa kodi iliyokusanywa ni shilingi 740,775,023.26 sawa na asilimia 16.
“ Idadi ya viwanja vilivyopimwa katika halmashauri zote ni 4,873 na mashamba 5 na mipango miji na vijijini ikiwemo michoro ya mipango miji 41 imepokelewa na kuhidhinishwa yenye jumla ya viwanjwa 18,581 vya matumizi mbalimbali “.
Ndemela amesema zoezi la kurasimisha makazi holela linaendelea katika halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma kwakuhusisha wataalaam wa ardhi waliopo katika halmashauri hizo ikiwemo Halmashauri ya Mbinga Mji pekee yenye kampuni moja ya upimaji smartGeo survey Co.LTD.
Hata hivyo amesema Pamoja najitihada za ofisi ya Ardhi Mkoa kwaajili ya kuongeza ufanisi katika utendaji kazi bado kuna changamoto ya wataalam katika halmashauri ya Madaba, Tunduru, Mbinga mji na Manispaa ya Songea, Pamoja naupungufu wa wenyeviti wa Mabalaza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Mkoawa Ruvuma unamabalaza 3 yaliyopo Songea,MbinganaTunduru balaza la Mbinga pekee lenyemwenyekiti.
Kamishina msaidizi amesema licha ya changamoto hizo ofisi ya ardhi Mkoa kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Halmashauri imeweka mikakati wa kurugenzi wenye upungufu wa wataalam wanaandika barua kwa katibu mkuu na kuwapatia wataalam kwa gharama za halmashauri husika, Kuhakikisha wadaiwa sugu wote wanapelekewa notisi za madai na kusambaza hati za madai na kuwafikisha mahakamani na
Kuhakikisha viwanja vilivyopimwa/vitakavyopimwa vinamilikishwa kulingana na matakwa ya mabadiliko ya Sheria ya ardhi,ambayo yanatoa mwogozo wa umilikishaji wamaeneno ambayo upimaji wake umekamilika na kuidhinishwa katika kipindi cha siku 90.
Imeandaliwana Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauriya Madaba
25,2,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa