SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia inatarajia kujenga Stendi ya Mabasi Madaba Mkoa wa Ruvuma na kupanua ujenzi wa soko linalojengwa kwa shilingi Milioni 190 kupitia mradi wa TASAF.
Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi Umma na Utalawala bora Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete walipotembelea Mkoa wa Ruvuma hususani Jimbo la Madaba.
Hata hivyo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal.Ahmed Abass Ahmed ambaye amewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri kwa kuwapokea na kufanikiwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa huo.
Kikwete amemaliza ziara Jimbo la Madaba iliyojumuisha Kamati ya kudumu ya Bunge utawala Katiba na Sheria katika stendi ya Madaba amewahakikishia kuwa Serikali italifanyia kazi suala la ujenzi wa Stendi hiyo.
“Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma tunashukuru sana siku mbili ya ziara yetu tumeona mengi na tumejifunza vingi katika Maeneo mengi sana kwa wananchi tuwahakikishie Serikali inayoongozwa na Rais Samia ametuelekeza tukasimamie maisha ya watu hususani ninyi wa Madaba na Nchi yetu kwa ujumla”.
Hata hivyo kwa niaba ya Serikali amemshukuru Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mbunge wa Jimbo hilo Joseph Mhagama kuwa maagizo yote kutoka kwa Wabunge watayafanyia kazi ikiwemo ujenzi wa stendi ya Madaba.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 14,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa