Leo Oktoba 13 Mahanje SACCOS wamefanya mkutano mkuu wa mwaka na kufanya uchaguzi wa viongozi wa wajumbe wa bodi,Kamati ya usimamizi na mjumbe mwakilishi wa mkutano mkuu Halamshauri ya Madaba.
Mzee mshauri wa Mahanje SACCOS Makaria Lupogo akizungumza mara baada ya uchaguzi huo amesema wanachama hao wahakikishe wanakopa na kulipa kwa wakati itapelekea kufanikisha malengo ya SACCOS hiyo.
“Siyo leo mnakopa halafu hamlipi mnahangaika kwenda kukopa kwingine sisi hii SACCOS imetulea na tumesomesha watoto wetu”.
Lupogo amewapongeza viongozi waliochaguliwa wafanye kazi na kuhakikisha SACCOS hiyo inasonga mbele.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mahanje Stephano Mahundi amesema amekuwa mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa SACCOS kwa kipindi cha miaka 6 na mjumbe wa kamati ya bodi kabla ya kuwa Diwani wa Kata ya Mahanje.
Mahundi amewaasa viongozi waliochaguliwa kuwa wamepewa nafasi ya kusimamia kazi ikiwa watu wengi wanaitazama hivyo wafanye kazi kwa weledi ili SACCOS hiyo iweze kufanya vizuri.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa