MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa amewasisitiza Waheshimiwa Madiwani Kusimamia Miradi ya Boost.
Hayo ameyasema katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu ya mwaka 2022/2023.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri Mwenyekiti amesema Waheshimiwa Madiwani wasimamie miradi ya Boost inayojumuisha ujenzi wa Madarasa ya Shule za Msingi na Awali na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
Afisa Elimu Vifaa na takwimu msingi Raphael Kibiligi ambaye ni mratibu wa Mradi huo amempongeza Rais Samia kwa kuleta fedha Milioni 610,300,000/= kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya Lipupuma na madarasa maalumu ya awali katika Shule ya Msingi Ifugwa pamoja na vyoo 6.
Hata hivyo Kibiligi amesema pia fedha hizo za mradi wa Boost zitatumika katika ujenzi wa madarasa 8 katika shule nne tofauti.
“Sisi kama Halmashauri tumejipanga kuhakikisha tunatekeleza mradi huu kwa wakati na kumaliza kwa wakati na kujenga majengo ambayo yataendana na thamani ya fedha ambayo tumepata”.
Kibiligi amesema mpaka kufikia sasa wametoa Elimu kwa jamii pamoja na kutamburisha mradi huo na baadhi ya maeneo wameshaanza kutekeleza mradi ikiwemo shule ya Lipupuma wameshaasafisha eneo la ujenzi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Matumbi Valentino Mtemauti ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia,kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya mradi wa Boost unaowezesha uboreshaji wa shule za msingi na awali.
Hivyo Mtemauti amewaomba Madiwani ambao fedha zimeenda katika Kata zao kuhakikisha wanasimamaia kwa weledi ili Halmashauri iendelee kuletewa fedha kwaajili ya miradi mingine ya Maendeleo..
Imeandailiwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Mei 19,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa