SHULE ya Msingi Mkwera Kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba wamefanya Mahafari ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la Saba 56 waliohitimu masomo yao mwaka huu 2023.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amewakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa amewapongeza wanafunzi hao kwa kuhitimu masomo yao kwa mda wa miaka 7.
Mlelwa amewapongeza walimu kwa kazi kubwa pamoja na kutoa maagizo kwa wanafunzi watakaofaulu wahakikishe wanajiunga na Elimu ya Sekondari Januari 2024.
“Niwapongeze walimu niliwahi kufika hapa Shuleni,Mazingira ya hapa ni masafi yanapendeza“.
Makamu Mwenye Kiti wa Halmashauri hiyo Olaph Pili ambaye ni Diwani wa Kata ya Lituta amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muunga wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya ukarabati wa Shule hiyo na ujenzi wa Madarasa Mapya shilingi Milioni 40.
“Shule hii ina Mazingira Mazuri ya Kusomea kwaajili ya Mapenzi ya Mama ameboresha mazingira haya“.
Hata hivyo Pili amesema Serikali ilileta Fedha kwaajili ya Ujenzi wa vyoo vya kisasa kupitia Mradi wa SWASH na kupelekea wanafunzi kupata mazingira Mazuri ya kujisomea hatimaye kufanya vizuri katika Mitihani ya Darasa la Nne na Darasa la Saba kwa asilimia 100.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa