HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wameadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Matetereka.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kijiji cha Matetereka Kata ya Matetereka,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa amekuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo.
Mlelwa amewataka wazazi na viongozi kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha mtoto anapata mahitaji na haki yake ya msingi.
Amesema kila tarehe 16 Mwezi Juni ni siku ya Kimataifa ya mtoto wa Kiafrika ambayo dunia inakumbuka watoto takribani 700 waliouawa wakati wa maandamano yaliyozua ghasia mji wa Soweto Afrika Kusini.
Hata hivyo amesema maandamano hayo yalizua taharuki na umwagaji wa damu yalijukana kama mauaji ya Soweto yaliyatumika kuhamasisha kwa jamii kuboresha mahitaji endelevu kama Elimu kwa watoto barani Afrika.
“Siku hiyo tarehe 16 mwaka 1976 zaidi ya wanafunzi 2000 wa Afrika kusini waliandamana mtaani wakitaka kuboresha Elimu ikiwemo kufundishwa kwa Lugha yao wenyewe baada ya lugha ya Kingereza na kuondoa mfumo wa ubaguzi wa rangi kwani uliowatenga wanafunzi weusi na wazungu “
Amesema ilipofika mwaka 1991 kutokana na uzito wa tukio lililoacha majonzi kwa jamii ya kiafrika na umoja wa OAU iliweka adhimio ya kuitambua siku ya tarehe 16 kila mwaka kuwa siku ya mtoto wa Afrika na kutambuliwa Duniani kote .
“Siku hii ya tarehe 16 Juni inalenga kuondoa vizuizi vinavyowakabili watoto wa Tanzania na Afrika kupata haki zao katika Nyanja zote ikiwemo Elimu bora,Afya,Malezi, ulinzi pamoja na kutokomeza ukatili dhidi ya watoto”
Halmashauri ya Madaba wameadhimisha kwa kauli mbiu isemayo ondoa vikwazo mwezeshe mtoto kutimiza ndoto zake,wakiungana na Waafrika wote kwa kujenga mifumo bora ya malezi itakayompa mtoto malezi bora huduma za Afya Elimu na haki zote za Msingi kama ilivyo katika sheria za Nchi na Kimataifa.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Matetereka Restuta Mgaya akisoma Risara katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika kwa Mgeni rasmi amesema kauli mbiu ya mwaka 2023 inayosema zingatia Usalama wa Mtoto katika ulimwengu wa kidijitali kupitia kauli mbiu hiyo walimu,wazazi na jamii wanatakiwa kufahamu madhara ya matumizi yasiyo sahihi ya mitandao kwa watoto.
Amesema matumizi ya mtandao kwa mtoto yanapelekea kwenda kinyume na sheria ya mtoto badala yake walindwe na kuongozwa kwenye matumizi ya vifaa vya kidijitali ikiwemo simu za mkononi,Runinga,Komputa na vishikwambi kwa sababu vifaa hivyo kupelekea maudhui yasiyofaa kwa watoto.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 16,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa