MWENYETIKI wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho ameipongeza Halmashauri ya Madaba kwa kupata Hati safi .
Akizungumza katika kikao maalumu cha baraza la Madiwani la kujadili utekelezaji wa hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema mafanikiao hayo yamepelekea nidhamu kwa wataalam na Madiwani kwa matumizi ya fedha za wananchi.
“Kati ya Halmashauri ambazo zimefanya vizuri kwa mda mrefu ni Madaba ,nichukue fursa hii kuwapongeza kwa dhati ya moyo wangu kwa kuendelea kupata hati safi “.
Mwisho ametoa rai kwa wataalamu na Madiwani kuendelea kutunza nidhamu pamoja na uaminifu katika utendaji kazi na kuuendelea kupata hati safi kwa miaka inayofuata.
Hata hivyo amempongeza Mwenyeki wa Halmashauri Teofanes Mlelwa kwa namna ambavyo anasimamia Halmashauri hiyo hasa usimamiaji na utekelezaji wa Miradi inayoletwa na Serikali kwa ubora na Viwango.
“Mara nyingi tukitembelea miradi na kukagua Halmashauri ya Madaba imekuwa na Miradi mizuri,inayoonyesha thamani ya fedha,na kumaliza miradi kwa wakati hongereni sana”.amesema Mwisho.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa