• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MWENGE wa Uhuru wazindua Madaba miradi ya Milioni 382

Posted on: April 14th, 2022

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge  wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma amekugua miradi minne na kuzindua miradi minne yenye thamani ya shilingi Milioni 382.3 katika Halmashauri ya Madaba Mkoani Ruvuma.

Akizungumza katika Mbio hizo amepongeza usimamizi wa miradi hiyo na kuwataka viongozi wa Halmashauri ya Madaba kuendelea kusimamia miradi hiyo ya Serikali.

Ndugu Geraruma amekagua mradi wa kikundi cha Maarifa Mtyangimbole, mradi wa Lishe Zahanati ya Magingo, mradi wa ugawaji vyandarua Zahanati ya Magingo pamoja na ugawaji wa pikipiki kikundi cha Umoja wa Madereva Bodabada Madaba.

‘’Ndugu zangu wenye watoto chini ya umri wa miaka mitano hakikisha unazingatia sana elimu kuhusiana na mapambano dhidi ya Malaria kwa kutumia vyandarua vyenye dawa, kuhudhuria clinic pamoja na matumizi bora ya Lishe’’, amesisitiza Geraruma.

Pia amezindua madarasa mawili shule ya sekondari Lipupuma, Klabu ya wapinga rushwa shule ya sekondari Magingo, madarasa matatu na ofisi shule ya sekondari Mahanje pamoja na Anwani za Makazi na Postikodi.

‘’Pongezi kubwa ziende kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba na pongezi hizo ni kwasababu ya marejesho ya fedha za maendeleo ya vijana alizozirejesha kwa wakati’’, amesema Geraruma.

Kwa upande wake Mkuu  wa Wilaya ya Songea  Mh Pololet Mgema amemshukuru kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa kuukimbiza Mwenge salama na ameahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa.

Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Madaba ulipokelewa tar 13/04/2022 na  ulikimbizwa jumla ya kilomita 247 na umepita katika vijiji 15, Kata sita na Tarafa moja.

Imeandikwa na Bahati Nyoni

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma 

Aprili 19 2022.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa