• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MWENGE wa Uhuru waridhia kuweka Mawe ya Msingi na kufungua miradi yote madaba

Posted on: April 20th, 2023

MWENGE wa Uhuru Kitaifa 2023 umeendelea na ziara yake katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ambapo Aprili 19,2023 umekagua na kuridhia miradi yote katika Halmashauri ya Madaba yenye thamani ya shilingi milioni 859

Miongoni mwa miradi iliyoridhiwa na Mwenge wa Uhuru ni mradi wa ujenzi wa maji katika Kijiji cha Mbangamawe ambapo serikali kupitia RUWASA imetoa zaidi ya shilingi milioni 545 kutekeleza mradi huo.

Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 ,Meneja wa RUWASA Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles amesema mradi huo ukikamilika kwa asilimia 100 utawawezesha wakazi 2,800 kupata maji safi na salama ya bomba.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo,Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Ndugu Abdalla Shaib Kaim amewapongeza RUWASA kwa  kuendelea kutekeleza miradi ya maji yenye viwango vinavyoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali.

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile kwa niaba ya wananchi amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowezesha kujenga mradi wa maji katika Kijiji cha Mbangmawe ambacho hakijawahi kuwa na maji ya bomba tangu kuanzishwa kwake.

Miradi mingine ambayo imetembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Madaba ni mradi wa lishe katika zahanati ya Likarangilo na mradi wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika Kijiji cha Magingo.

Mwenge wa Uhuru pia ulikagua mradi wa utunzaji mazingira na kutembelea chanzo cha maji katika hifadhi ya misitu ya Wino inayosimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS),ambapo Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru amepongeza kazi kubwa inayofanywa na TFS kwenye utunzaji mazingira nchini.

Katika Halmashauri ya Madaba pia Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi kwenye mradi wa nyumba ya kulala wageni katika Kijiji cha Lilondo iliyojengwa na Mwananchi binafsi Ibrahimu Kilangwa kwa gharama ya shilingi milioni 126.

Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika Halmashauri ya Madaba pia ameweka jiwe la msingi katika kikundi cha  Kwetu Madaba ambacho kimepewa mkopo na Halmashauri shilingi milioni 44 kufanya mradi wa kufyatua tofali za saruji.

Mwenge wa Uhuru pia umekagua na kufungua rasmi vyumba viwili vya madarasa vyenye thamani ya shilingi milioni 40 katika sekondari Madaba.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa