HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya kikao cha wadau wa Mwenge wa Uhuru unaotarajia kufika Mkoa wa Ruvuma Aprili 17.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akizungumza katika kikao hicho amesema lengo la kuwaita wadau ili kuwaeleza juu ya Mwenge wa Uhuru unaotarajia kufika katika Halmashauri hiyo Aprili 19 na kukagua pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
“Aprili 19,2023 tutaupokea Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri yetu ya Madaba kutoka Wilaya ya Namtumbo namapokezi yatafanyika katika Shule ya Msingi Likalangiro Kata ya Mtyangimbole”.
Mkurugenzi amesema kuanzia sasa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri hiyo umeanza kwa kuandaa miradi na uhamasishaji kwa wananchi ili wajue tukio muhimu linakuja.
“Sisi kama wadau na viongozi tukawaambie wananchi Mwenge wa Uhuru unakuja katika Halmashauri yetu ya Madaba,kwa maana hiyo kupitia Mwenge wa uhuru unamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hii ni heshima kubwa katika Halmashauri yetu”.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa katika kikao hicho cha wadau amesema amefurahishwa na ujio wa wadau kwa kushiriki Kikao hicho ikiwa linapotokea jambo la muhimu kama Mwenge wa Uhuru kuwe na ushirikishwaji kwa wanadu mbalimbali na wananchi.
“Mwenge wa uhuru unapokuja katika Maeneo yetu unapita kwenye miradi ambayo ni yawananchi tuhakikishe tunakesha nao wote tumeona vema kuwakaribisha wadau kwa kutii na kuja”.
Mlelwa ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku hiyo ya kuupokea Mwenge wa Uhuru bila kupuuza ikiwa Mwenge unakuja kwaajili ya wananchi wote siyo viongozi wa Serikali pekee.
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la KKT Madaba Faraja Kisosho katika kikao hicho cha Wadau amewapongeza viongozi wa Serikali kwa kutambua umuhimu wa kufanya kazi na viongozi wa Dini kushirikishwa katika mambo ya kiserikali.
Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi kuwa siku ya Mkesha wa Mwenge wa Uhuru wananchi wawe na maadili ili kuhakikisha zoezi hilo linaenda vizuri.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 14,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa