MWENYEKITI wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho amekabidhiwa vitanda 20 vilivyotolewa na mwekezaji wa Kijiji cha Ifinga kampuni ya Mufindi Woodpoles planting and Timber Ltd.
Awadhi nyagongo akiwakilisha kampuni hiyo amesema wametoa msaada wa vitanda hivyo kwaajili ya kumaliza changamoto za wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ifinga.
Hata hivyo Kampuni hiyo imetoa shilingi Laki nane kwaajili ya ukarabati wa Ofisi ya Tawi la chama cha Mapinduzi Ifinga.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ifinga Agustino Mbawala amesema shule hiyo inajumla ya wanafunzi 80 kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.
Moja ya wanafunzi wa shule hiyo Rehema Gwide amemshukuru mwekezaji huyo kwa kuwapa vitanda ikiwa kabla walikuwa wanatumia kitanda kimoja wanafunzi watatu.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 9,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa