Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewakilishwa na Katibu tawala Wilaya ya Songea Mtela mwampamba ameongoza kikao cha Kujadili na kutoa maoni ya Dira yaTaifa ya maendeleo ya mwaka 2026/2050.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ikijumuisha Halmashauri tatu za Wilaya ikiwemo Manispaa ya Songea,Halmashauri ya Songea na Madaba.
Mwampamba akizungumza katika kikao hicho cha kutoa maoni amesema dira ni mwongozo unaowafanya Watanzania waishi kwa mtindo waliouweka katika kuongoza Taifa.
“Dira ya Taifa ya maendeleo inaweza kuwa ya mda mfupi miaka mitano,mda wa kati miaka 25, na mda mrefu miaka 50 hadi 75”.
Amesema katika nchi ya Tanzania mara baada ya kupata Uhuru 1961 hakukuwa na dira ya Taifa ya maendeleo kilichokuwa kinafanyika ni kuhakikisha mambo yanafanyika kulingana na wakati uliopo.
“Wazee wangu mnajua kwamba tulikuwa na sera zetu na maadhimio ya Arusha ,kilimo hatukuwa na dira ya Taifa ya maendeleo ya kutuongoza tulipofika mwaka 1980 tuliona tuwe na dira ya Taifa”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 12,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa