MVUA iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha takribani dakika 10 Machi 12,2024 majira ya jioni imeezua madarasa mawili na vyoo katika shule ya Msingi Likarangiro na nyumba moja ya mwananchi Kata ya Mtyangimbole Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri hiyo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Sajidu Idrisa Mohamed amewakilishwa na Joseph Mrimi Mkuu wa Idara ya Kilimo wamefika katika eneo hilo kuhakikisha wanakarabati madarasa hayo ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Likarangiro Rajab Mipango Mpumila amewashukuru viongozi hao kwa kufika katika eneo la tukio kwa wakati na kuwahakikishia kufanya zoezi la ukarabati wa madarasa ambayo yameezuliwa na upepo ili wanafunzi waweze kurejea madarasani.
Kutoa Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 13,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa