Muhifadhi Msaidizi wa Shamba la Miti Wino Halmashauri ya Madaba Godfrey Shio ametoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari ya Moto kwa kipindi hiki cha Kiangazi.
Hayo amezungumza katika Mahafari ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Wilima amesema imekuwa janga kwa wananchi wanaowekeza katika kilimo cha Miti na kupata hasara ya kuteketea kwa Moto.
“ Watu wengi wanawekeza katika mashamba ya Miti halafu watu wanachoma moto hovyo hivyo kuteketeza malizao tunaomba mchukue tahadhari”.
Hata hivyo shio amema wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka shamba la Miti Wino wanakaribishwa kujipatia miche ya miti bure.
Amesema mwananchi anapaswa kuandika barua na idadi ya miche anayohitaji , namba ya ya simu pamoja na eneo analopanda na kuwasilisha kwa muhifadhi wa shamba hilo.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmshauri ya Madaba
Oktoba 14,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa