Muhifadhi Mkuu wa Shamaba la Miti Wino Halmashauri ya Madaba Grory Fotunatus amesema shangamoto zinazolikabili shamba hilo ukiwemo uchomaji wa moto.
Hayo amesema katika kikao cha wadau wa Misitu kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas ambapo amewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile.
Hata hivyo amezitaja changamoto ya moto inayosababisha kupunguza jitihada za usimamizi wa Shamaba ikiwemo msimu wa kilimo ikiwa mwaka 2016 ziliungua hekta 600 na 2020/2021 ziliungua hekta zaidi ya 1000.
Amesema changamoto hizo zilisababishwa na uandaaji wa mashamba ikiwa mwaka huu 2023 kikosi kilipambana na moto na watu wanne walipata ajali ya moto na mmoja alipoteza maisha baada ya kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na watatu bado wanapatiwa matibabu.
Fotunatus amesema katika kukabiliana na janga hilo la moto uongozi wa shamaba wamejitaidi kutoa Elimu na vifaa mbalimbali kwa jamii mawasiliano baina ya uhifadhi na wananchi.
“Tumekuwepo na kikosi maalumu cha kupambana na kuzuia moto pindi unapotokea na kufanya kazi za kinga moto ndani ya shamba na nje ya shamba katika kuboresha na kuhakikisha moto hautokei ndani ya shamba”.
Amesema shamba la miti Wino linaendelea kuwaomba wadau kuepuka kuchoma moto maeneo hatarishi wakati wa uandaaji wa shamba na kuwataka kufanya maandalizi mazuri ya barabara kinga moto.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 12,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa