Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametoa ufafanuzi wa mabadiliko ya tarehe ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi na ukomo wa viongozi wa Serikali za mitaa za vijiji pamoja na masuala ya uapishaji wa mawakala.
Ufafanuzi huo ameutoa katika kikao na viongozi wa vyama vya siasa katika halmashauri hiyo kuendea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakao fanyika Novemba 27,2024.
Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi amesema maoni mbalimbali yanayoendelea kutolewa na wadau, nayo Serikali imeendelea kutoa miongozo mbalimbali pamoja na kusisitiza matumizi sahihi ya Sheria za uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa uhuru na haki.
Aidha amezitaja tarehe za mabadiliko ikiwemo fomu za uteuzi kwa wagombea zitaanza kutolewa na kurejeshwa kuanzia Oktoba 26 ,2024 hadi Novemba 1,2024 badala ya tarehe 1,hadi 7 Novemba.
“Ukombo wa viongozi wa Serikali za Vijiji ratiba ya awali ulionyesha oktoba 25,2024 hivyo uongozi wa Serikali za Vijiji utakoma oktoba 19,2024 hii ni kutoa fursa viongozi madarakani kuweza kupata fursa ya kuchukua fomu kwa wakati na kurejesha kwa wakati”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa