MSIMAMIZI wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametoa maaelekezo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa wasimamizi ngazi ya vijiji,Kata , Halmashauri,na wawakilishi wa vyama vya siasa pamoja na viongozi wa dini.
Zoezi hilo limetolewa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ikiwa ni takwa la kisheria la kuwajulisha wananchi kupata maelekezo siku 62 kabla ya tarehe ya uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa kwa wapiga kura na wagombea.
Hata hivyo amezitaja tarehe muhimu za kujiandikisha katika daftari la kudumu na tarehe za kuanza kwa kampeni na tarehe ya uchaguzi utakaofanyika mwaka huu 2024.
“Zoezi la kujiandikisha katika daftari la wapiga kura litaanza Oktoba 11 hadi 20,2024,Kampeni zitaanza Novemba 20 hadi 26,2024 na uchaguzi utafanyika Novemba 27,2024”.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa na kuzingatia kila jambo linalohusu uchaguzi kwa utulivu na kuzingatia 4R za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan.
Nao viongozi wa vyama vya Siasa wilioshiriki katika zoezi hilo wametoa pongezi kwa kushirikishwa na kupewa taarifa kwa wakati hivyo wameahidi kwenda kutekeleza yote yanayopaswa kutekeleza na kutoa ushirikiano kwa amani na utulivu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Septemba 26,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa